Tovuti rasmi ya serikali ya Marekani

Kuhusu

Mazoea bora zaidi ya TOR

Kuna njia nyingi kuongeza usalama wako wakati ukitumia kivinjari cha mtandao The Onion Router (TOR). Mbali na kutumia TOR, tunapendekeza kutumia huduma za mitandao binafsi inayoaminika (VPN) ili kuimarisha zaidi usalama wa trafiki yako mtandaoni. Kwa kuunganisha na mahali iliyopo seva nje ya nchi yako kabla ya kutumia TOR, trafiki yako mtandaoni inalindwa zaidi kutokana na ufuatiliaji. Ndani ya kivinjari cha mtandao cha TOR, kuna mipangilio zaidi iliyopendekezwa katika sehemu ya “usalama na uthabiti”ndani ya TOR. Kwanza, wezesha VPM. Halafu:

  1. Anzisha kivinjari cha mtandao cha TOR
  2. Ingia kwenye mipangilio ya TOR na chagua “Faragha na Usalama”
  3. Chagua kisanduku “Futa vidakuzi na data ya tovuti kivinjari cha mtandao cha TOR kinapofungwa”
  4. Sogea chini kwa sehemu ya Historia: Badilisha mpangilio kuwa “Usikumbuke kamwe historia”
  5. Sogea chini kwa Ruhusa: bofya mipangilio ya kamera bofya “Zuia maombi mapya yanayoomba kufikia camera yako.” Fanya vivyo hivyo kwa mikrofoni. Kwa usalama zaidi funika kamera yako ya mbele kwenye kifaa chako kwa kutumia tepu au kizuizi.
  6. Sogea kwa usalama: bofya “Salama Zaidi” Hii itazima utendakazi Fulani ndani ya TOR lakini itawezesha muunganisho salama zaidi.
  7. Sogea kwa Modi ya HTTPS-Pekee: Bofya Wezesha modi ya HTTPS-Pekee kwenye madirisha yote. Hii itahakikisha kwamba miunganisho yako yote imesimbwa na ni salama.
  8. Ingia mpangilio wa “TOR” chini ya “Faragha na Usalama”
  9. Chagua kisanduku “Tumia daraja”
  10. Bofya “Omba daraja kutoka torproject.org”
  11. Weka jibu la kukutambulisha wewe ni binadamu (captcha).
  12. Tumia https://coveryourtracks.eff.org na https://ipleak.net kuona ni taarifa gani za utambulisho labda bado zipo ambazo zinaweza kwa kipekee kunasa alama mahususi ya kompyuta yako na trafiki ya wavuti.

Njia salama kuunganishwa na TOR na laini ya vidokezo ya Tuzo ya Mahakama TOR

  1. Tumia huduma ya VPN inayoaminika uliyoilipia wewe. Huduma bure za VPN huenda zikawa sio salama wakati wote.
  2. Unganisha kifaa chako kwa kutumia huduma ya VPN inayoaminika na mahali nje ya nchi ambapo unafikia TOR.
  3. Anzisha kivinjari cha mtandao cha TOR
  4. Sanidi mipangilio ya usalama ya TOR unavyoona inafaa.
  5. Kwa usalama zaidi, tumia mfumo wakilishi halisi kama wa duka la kahawa au ukumbi wa hoteli ili muunganisho usiweze kutambua mahali halisi nyumbani kwako.

Viungo kwa taarifa za usalama na uthabiti za TOR

  1. Taarifa kuhusu Madaraja ya TOR: https://tb-manual.torproject.org/bridges/.
  2. Taarifa kuhusu usalama wa TOR: https://tb-manual.torproject.org/security-settings/.

SUBMIT A TIP

Do Your Part. Secure a Safer World.

There are many ways to submit information to Rewards for Justice.

You may choose from multiple platforms and contact us in numerous languages. To process your information efficiently, we ask you to state your information as succinctly as possible, provide your name, location, and preferred language, and upload all relevant files such as photographs, videos, and documents to support your information. An RFJ representative will soon contact you. Please be patient, as RFJ reads every tip we receive.

Please open your Line app to submit a tip. The number is +1 202 702 7843

Please open your Viber app to submit a tip. The number is +1 202 702 7843

Please visit our Tor-based tips-reporting channel at: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Wasilisha Kidokezi

Fanya Jukumu Lako - Dhamini Ulimwengu Salama Zaidi

Zipo njia nyingi kuwasilisha kidokezo.

Unaweza kuchagua kutoka majukwaa mengi na kuwasiliana nasi katika lugha nyingi.
Kuchakata taarifa yako kwa ufanisi, tunakuomba kusema taarifa zako kwa maneno mafupi na Dhahiri iwezekanavyo, kutoa jina lako, mahali uliko, na lugha unayopendelea, na kupakia faili zote husika kama vile picha, video, na hati kuunga mkono taarifa yako. Mwakilishi wa TKM atawasliana nawe hivi karibuni. Tafadhali uwe na Subira, kwa kuwa TKM husoma kila kidokezo tunachopokea.

Tafadhali fungua programu yako ya Line ili kuwasilisha kidokezo. Nambari hiyo ni +1 202 718 4649

Tafadhali fungua programu yako ya Viber ili kuwasilisha kidokezo. Nambari hiyo ni +1 202 718 4649

Tafadhali tembelea idhaa yetu ya kuripotia vidokezo inayotumia mfumo wa TOR katika: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Skip to content